Na GLADNESS MALLYA
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Baby Joseph Madaha amenusurika kubakwa nchini Kenya baada ya kupanda jukwaani akiwa ametinga kivazi cha nusu utupu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Baby Joseph Madaha akipozi.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika mji wa Naivasha uliopo
Nairobi nchini humo ambapo mwanadada huyo alipopanda jukwaani akiwa
amevaa sketi fupi iliyokuwa imeacha sehemu kubwa ya mapaja wazi, wanaume
wakware walianza kumvutia chini kwa nguvu.
Baby Madaha akifanya shoo na kunengua jukwaani akiwa ametinga sketi fupi.
“Nusura Baby Madaha abakwe, wanaume wakware walishindwa kuvumilia,
palepale jukwaani wakaanza kumvuta huku wengine wakimng’ang’ania paja
lake lakini aliokolewa na mabaunsa vinginevyo tungekuwa tunaongea
mengine,” kilisema chanzo.
Baby madaha akizidi kuwapagawisha wakenya.
Ijumaa limezinasa picha kadhaa zinazomuonesha Baby Madaha akiwa
anang’ang’aniwa na wanaume tofauti huku wengine wakimchungulia sehemu
zake ‘muhimu’ pamoja na kumshika mapaja yake.
Wanaume wakiung'ang'ania mguu wa Baby madaha.
“Kweli ilikuwa ni hatari siku hiyo maana wanaume waliniganda balaa
kila nilipokuwa naimba jukwaani walikuwa wakinivutia kwa huku chini
walikokuwa wamesimama lakini niliokolewa na mabaunsa, hata hivyo shoo
ilikuwa na mzuka sana,” alisema Baby Madaha.
Baby Madaha akiwa ameanguka chini baada ya kuvutwa na watazamaji waliokuwa karibu na jukwaa.
Baby Madaha akipata akiwa na baadhi ya mastaa kutoka Kenya.
Kwenye shoo hiyo iliyokuwa na nyomi ya kutosha, Baby Madaha alikamua
vilivyo sambamba na wasanii wakali kutoka Kenya akiwemo Jua Kali na
Wayree






0 comments
Post a Comment