Stori: Rhoda Josiah
WAKATI wasanii mbalimbali wakijumuika pamoja katika kisomo cha kuwakumbuka
marehemu kilichotayarishwa na Bongo Movie jijini Dar juzikati, mdada anayefanya poa kwenye anga la filamu, Devota Mbaga, amejikuta kwenye simanzi nzito akiwakumbuka Mzee Small na Adam Kuambiana, akisema walikuwa watu wake wa karibu aliotoka nao mbali.
Mdada anayefanya poa kwenye anga la filamu, Devota Mbaga.
“Siku ya leo ni kumbukumbu ya pigo zito kwangu, maana nikimzungumzia
Kuambiana, nilijuana naye kitambo sana kabla hata mambo ya vyama hayapo,
Mzee Small alikuwa mtu muhimu sana kwangu hata alipoanza kuugua
nilikuwa naye bega kwa bega nikimsaidia, wapumzike kwa amani kwa
kweli,”alisema Devota.Posted byMr.Prime on August 20, 2014
0 comments
Post a Comment