‘We Talking Money You Talking Nonsense’ huenda ikawa kauli nzuri kuelezea hiki walichokifanya P-Square kwa sasa.
Hakuna
ubishi kuwa, kwa hiki walichokifanya sasa, na kama macho yetu
hayatudanganyi kwa hiki yanayokiona, mapacha hawa wamefanya kufuru. Kama
hii inayoonekana ni dhahabu kweli, basi P-Square, hela wanayo.


Peter ameshare picha hizi nne ambazo
wiki hii zitakuwa gumzo barani Afrika ambapo kwenye picha moja
inayomuonesha pacha mwezie Paul akiwa amesimama kwenye sebule mpya
inayoaminika kuwa ya nyumba yao mpya, ameandika ‘Goldenworld #blessed.’

Kwenye picha nyingine, wanaoonekana
wakiwa pamoja kwenye sebule hiyo iliyotawaliwa na kile kinachoonekana
kama dhahabu zilizozunguka sofa za kuvutia na Peter ameandika: #2kings……
Work hard,play harder.’

0 comments
Post a Comment