Stori: Chande Abdallah, Deogratius Mongela na Shani Ramadhani
MATUKIO ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa watoto yamekuwa
yakiendelea kufanyika kila siku licha ya kukemewa mara kwa mara, safari hii, baba na mama wakidaiwa kumsulubu mtoto wao.
Katika hali ya kuonesha kwamba vitendo hivyo bado vinaendelea kwa kasi, familia moja iliyopo Kunduchi jijini Dar imeshikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za ukatili dhidi ya mtoto baada ya kudaiwa kumsulubu kwa vipigo mfululizo mtoto wake aliyejitambulisha kwa jina la Fadhili (10).
Mtoto anayetambulika kwa jina la Fadhili amekuwa akifanyiwa unyama na baba na mama yake wa kambo.
Chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa mbali na vipigo hivyo, mtoto
huyo amekuwa akinyimwa chakula na kudaiwa kung’atwa meno na mdogo wake
sambamba na kutakiwa kunywa mkojo wake ikiwa ni adhabu ya makosa
anayoyafanya.
Majeraha ya mkononi aliyoyapata mtoto Fadhili kutokana na unyama wa baba na mama yake wa kambo.
“Yaani anayofanyiwa mtoto huyo ni ukatili mkubwa, tena nje ya umri
wake, inafikia hatua hatazamiki kutokana na majeraha yaliyopo mwilini
mwake. Mbaya zaidi hasomi shule na amekuwa mlezi wa baba yake ambaye
amepooza,” kilisema chanzo hicho kilichoiomba OFM iingilie kati kwa kuwa
suala hilo lilishawahi kuripotiwa kwenye ngazi ya serikali ya mtaa bila
kufanyiwa kazi.
Majeraha mengine sehemu juu ya mkono.
Timu ya Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’
ilifika eneo la tukio kuhakikisha taarifa hizo ambapo ilibahatika
kuzungumza na mtoto huyo ambaye alikiri kufanyiwa ukatili huo na wazazi
wake.
OFM ilishuhudia makovu mengi mwilini mwake jambo liliwafanya kufika kwenye Ofisi ya Mtendaji Kata ya Kunduchi ambao waliambatana hadi nyumbani kwa mtoto huyo.
OFM ilishuhudia makovu mengi mwilini mwake jambo liliwafanya kufika kwenye Ofisi ya Mtendaji Kata ya Kunduchi ambao waliambatana hadi nyumbani kwa mtoto huyo.
Majeraha ya meno mkononi.
Baba mzazi wa mtoto huyo alikataa katakata madai ya mkewe kumtesa mwanaye.“Mke wangu hahusiki na huyu mtoto, mimi ndiye nitakwenda kuyajibu hayo mashtaka kwa kuwa ni wangu na huyu si mama yake, kama shule nimemsimamisha ili anihudumie hapa nyumbani kwa kuwa nimepooza,” alisema baba huyo.
Baba mzazi wa mtoto Fadhili akiwa na mke wake .
Hata hivyo jitihada za kuwafikisha ofisi ya mtendaji zilishindikana
baada ya familia hiyo kuona ikiandamwa na OFM, lakini baadaye
walijisalimisha wenyewe na kufikishwa kituo cha Polisi cha Kawe ambapo
walifunguliwa mashtaka kwa jalada KW/RB/6720/14 UNYANYASAJI.





0 comments
Post a Comment