Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, akihutubia
wakati
akifunga Kongamano la 25 la Wajiolojia Barani Afrika
lililofanyika tarehe 14-16 Jijini Dar es Salaam. Wakati akifunga
Kongamano hilo, Waziri Pinda amewataka watafiti barani Afrika kufanya
tafiti ambazo zina mahusiano ya moja kwa moja na jamii ili tafiti hizo
zitumike katika kuwazesha wananchi kufaidika na rasilimali zilizopo
barani Afrika.Baadhi ya Wajilojia kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wanaohudhuria Kongamano la 25 la Wajiolojia Afrika wakifuatilia hotuba ya kufungamano hiyo iliyosomwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani)
.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajiolojia waliohudhuria kongamano hilo kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Sadik Meck Sadik na Rais wa Wajolojia Afrika Profesa Aberra Mogassie.
Na Asteria Muhozya, Dar es SalaamWaziri Mkuu Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajiolojia waliohudhuria kongamano hilo kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Sadik Meck Sadik na Rais wa Wajolojia Afrika Profesa Aberra Mogassie.
Wanajiolojia barani Afrika wametakiwa kufanya tafiti zenye uhusiano wa moja kwa moja na jamii na kuzionesha tafiti hizo ili ziweze kutumiwa kama ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yanayolikabili bara hilo, jambo ambalo litaiwezesha Afrika kunufaika na rasilimali zilizopo na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi , maendeleo ya watu na mapato ya mataifa yao.
“Najua watafiti wanaweza kusema serikali zetu hazitumii tafiti zetu, lakini mkifanya tafiti zenye uhusiano wa moja kwa moja na jamii, mkazitoa kwa jamii tutazitumia msizifungie makabatini,” amesisitiza Pinda.
Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda leo jijini Dar es
Salaam wakati akifunga kongamano la 25 la Wanajiolojia barani Afrika na
kueleza kuwa, ili Afrika iweze kuendelea na kufaidika na rasilimali
zake, inahitaji kuzalisha wataalamu wengi katika taaluma ya sayansi
ikiwemo wanajiolojia.
“Hapa nchini Tanzania Profesa Muhongo
anapambana sana na taaluma hii, jambo hili litasaidia kuzalisha
wataalamu wengi katika sekta za mafuta na gesi. Lakini na ninyi,
mnahitaji kuzalisha wataalamu ili tuisogeze mbele Afrika,” alibainisha
Pinda.
Ameongeza kuwa, serikali ya Tanzania tayari
inajipanga katika kuhakikisha inazalisha watalaam wengi wa sayansi
kupitia programu za Vyuo Vikuu ambapo tayari imeanzisha masomo ya mafuta
na gesi katika baadhi ya vyuo vikuu nchini, hususani Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu Dodoma (UDOM), ikiwemo kampeni ya
kuhakikisha kwamba kila shule ya sekondari inakuwa na maabara ambazo
zitachochea kizazi cha wanasayansi.
Vilevile, amezungumzia tatizo la Afrika
kutokufaidika na rasilimali zake zilizoko ardhini na kuongeza kuwa,
linatokana na matumizi kidogo ya sayansi yanayofanywa na nchi nyingi za
Afrika, hivyo, amewataka wataalamu hao kuhakikisha wanatoka na njia
ambazo zitasaidia na kuliwezesha bara hilo kuitumia sayansi kwa
maendeleo ya nchi zao kwa sasa na kwa kizazi kijacho.
Aidha, amewataka wataalamu hao kutumia
kuitumia taaluma hiyo zaidi ya inavyotumika sasa ikiwemo kuhakikisha
kwamba afrika inasimama imara kupitia rasilimali zilizopo na kuiondoa
katika matatizo ya kiuchumi, kiafya na kimazingira.
Halikadhalika, amewataka wataalamu hao,
kufikiria namna ambavyo nchi za afrika zitasimamia suala la
uthaminishaji madini katika nchi zao kwa kuhakikisha kwamba, shughuli za
uthamini madini zinafanywa ndani ya Afrika tofauti na sasa ambapo nchi
nyngi bado zinasafirisha madini nje bila kuyathamini jambo ambalo
linachangia katika kuzikosesha nchi hizo mapato stahiki yanayotokana na
rasilimali hiyo.
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza katika mkutano huo,
amewataka wajilojia Afrika kufanya tafiti nyingi za kutosha ili kujua
kiasi cha mafuta na gesi ambacho bado kipo Afrika lakini bado
hakifahamiki ili rasilimali hizo zisaidie kubadilisha taswira ya
afrika.
Ameongeza kuwa, Afrika inatakiwa kujikita
zaidi katika kuzalisha wataalamu wa kutosha na kujua namna ya
kuziendelea rasilimali hizo wakati huo huo ikihakikisha kwamba,
zinchangia kwa kiasi kikubwa katika kuinua uchumi, kuvutia uwezaji na
kuchangia katika maendeleo ya watu.
Ameongeza kuwa, bado afrika inazalisha
kiasi kidogo cha nishati ya umeme wakati dunia inahitaji nishati hiyo
kwa kiasi kikubwa hivyo, amewataka wataalamu hao kuhakikisha wanasaidia
katika kuwezesha upatikanaji wa rasilimali hiyo kupitia taaluma zao.
Vilevile, amewataka wajiolojia afrika kuipa
kipaumbele miradi ya umeme vijijini katika nchi zao, na kuhakikisha
kwamba, miradi hiyo kama ilivyo miradi ya REA nchini, inafanyika na
kufanikiwa kwa kiasi kikubwa ikiwemo kufanya tafiti kuhusu miradi hiyo.
Katika hatua nyingine, Profesa Muhongo
amekitaka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu Dodoma kulifanyia
kazi suala la ukosefu wa wahadhiri katika vyuo hivyo katika fani za
mafuta na gesi na wizara imehaidi kuhakikisha kwamba inawezesha
upatikanaji wa wakufunzi katika masomo hayo kutoka sehemu mbalimbali
duniani.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam Profesa Nelson Boniface, ameeleza kuwa, kongamnao hilo la siku
tatu la wajiolojia barani Afrika limewawezesha washiriki kujadili
masuala mbalimbali yanayoihusu taaluma hiyo yakiwemo kyanayohusu
nishati mchanganyiko, namna ya namna jilojia inavyoweza kusaidia
matatizo ya umaskini, maji, afya na mengineyo yalijadiliwa katika
kongamano hio.
Profesa Boniface ameongeza kuwa, washiriki
wa kongamano hilo walijadili na kuona kwamba, uwepo wa wataalamu
waliobobea katika taaluma hiyo ni jambo la msingi kutokana na nafasi na
mchango wao katika kuendeleza , namna ya kutumia Afrika na dunia
zinavyoweza kufaidika na rasilimali hizo.
Akielezea kuhusu mkutano wa Tatu wa
Wanasayansi Vijana Duniani ambao ulitangulia kabla ya kongamano hilo,
ameleza kuwa, mkutano huo uliweza kuwapa nafasi vijana kujadili masuala
mbalimbali kuhusu namna jiolojia inavyoweza kuchangia kuondoa umaskini
na kuwezesha maisha bora kwa jamii ya Afrika inavyoweza kunufaika na
rasilimali asilia na masuala mengine muhimu.
Kongamano la 25 la Wajilojjia Afrika
limewakutanisha wajiolojia waliobobea katika taaluma hiyo kutoka nchi
zaidi ya 42 Afrika na duniani . Aidha, Serikali kupitia Wizara ya
Nishati na Madini imewezesha kufanyika kwa kongamano la wajilojia
uliokuwa ufanyike nchini Brazil.
Aidha, mikutano yote miwili imedhaminiwa na
taasisi na makampuni mbalimbali, ambapo pia kampuni inayofanya utafiti
na uchimbaji wa gesi na mafuta ya BG-Tanzania ilikuwa ndio mdhamini mkuu
wa kongamano hilo.
kongamano lingine la Wanajiolojia Afrika linatarajiwa kufanyika nchini Afrika kusini.
0 comments
Post a Comment