Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Mhe Samwel Sitta, alipowasili kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 19, 2014. Kulia ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora), Mhe George Mkuchika akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi
 
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwenye ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM Dodoma Agosti 19, 2014. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.Kulia ni Makamu wa CCM (Bara) Ndg Philip Mangula akifuatiwa na Katibu Mkuu wa
CCM Ndg Abdulrahman Kinana
 
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa katika Uwanja wa ndege wa Dodoma na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt Emmanuel Nchimbi
 
Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Songea mjini Dkt Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Mbunge wa jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama, na Naibu Waziri wa Fedha na mbunge wa Iramba Magharibi Mhe Mwigulu NchembaPosted by Mr.Prime on August 20, 2014

0 comments

Post a Comment