Stori: Mayasa Mariwata
Si kweli! Mtoto mzuri Bongo Movies, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amekanusha vikali madai ya kutembea
na pedeshee mmoja anayedaiwa kuwa ni mmiliki wa baa moja iliyopo maeneo ya River-Side, Ubungo jijini Dar.
Mtoto mzuri Bongo Movies, Jennifer Kyaka ‘Odama'.
Baada ya kusomewa madai hayo ambayo yamesambaa kwenye mitandao ya
kijamii, Odama alikanusha vilivyo na kusema wanamsingizia tu.“Hee! Mbona
huyo mtu wala simjui, ndiyo kwanza nazisikia hizo habari wakizikuza
kwenye mitandao,” alisema Odama.
Odama 'akijiweka fiti'.
Kwenye madai hayo mtandaoni, Odama anadaiwa kuwa hajatulia na ndiyo
sababu ya kutomwanika baba mtoto wake, jambo ambalo mwenyewe amesema si
kweli bali ni utaratibu wa maisha yake aliojiwekea wa kutomuanika mzazi
mwenzake.Posted by Mr.Prime Limited Company on August 19, 2014
0 comments
Post a Comment