WATOTO WAMKUMBUSHA UYATIMA NISHA

Posted by Posted by Unknown On 23:30


                                        
Stori: Rhoda Josiah
MWANADADA anayefanya vizuri katika kiwanda cha filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema
watoto wanamkumbusha namna alivyoishi akiwa yatima, hivyo anawapenda sana.
 
Msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Nisha alitoa kauli hiyo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar juzikati wakati wa hitima ya kuwakumbuka marehemu ambapo Nisha alionekana kuwa kivutio kwa watoto waliofika viwanjani hapo kwa ajili ya kaswida, kwani mara baada ya kisomo kumalizika, watoto hao walimfuata na kucheza naye.
“Kiukweli, nimefurahi sana kucheza nao kwani watoto ndiyo watu pekee wanaonipa furaha katika maisha yangu kwani mimi ni mtoto yatima,” alisema.
                                                     Posted by Mr.Prime on August 20, 2014

0 comments

Post a Comment