Na Shakoor Jongo
Yule zilipendwa wa sexy lady wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe aitwaye Ramadhan Abdallah Mtoro ‘Dallas’ anadaiwa kukumbuka
shuka kukiwa kumeshakucha ikielezwa kwamba eti anabembeleza kurudiana na staa huyo waliyetengana takriban mwaka mmoja uliopita ili wakamilishe taratibu za kufunga pingu za masha.
Ramadhan Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
Akizungumza na Amani hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Lango la Jiji
uliopo Magomeni, Dar, Dallas alisema kuwa anamshangaa Wolper kumkatalia
ombi lake la kurudisha uhusiano wao wa kimapenzi huku akijua fika kuwa
bado anampenda. “Nampenda sana Wolper. Pliz namuomba turudiane tu.Ningejua kipindi kile nilivyorudi kutoka nje ningefunga naye ndoa kwani sasa hivi angekuwa ni mke wangu niliyechaguliwa na Mungu lakini ndiyo hataki,” alisema Dallas. Kwa upande wa Wolper alisema kuwa Dallas kwa sasa ni mshikaji wake tu na atabaki kuwa hivyo lakini kuhusiana na mapenzi, hakuna kitu kama hicho.
Sexy lady wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe.
“Nitasaidiana naye kwa kitu kingine lakini siyo mapenzi, kwa sasa
niko na mtu wangu,” alisema Wolper. Kabla ya jahazi kwenda mrama, penzi
la Wolper na Dallas lilitikisa mji huku kukiwa na maneno mengi ambayo
yalimshinda mkali huyo wa filamu za Kibongo ambaye aliamua kuchukua
hamsini zake.

0 comments
Post a Comment