Na Richard Bukos
BEAUTIFUL Onyinye, Wema Sepetu ametangaza dau la shilingi milioni moja kwa
yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa mbwa wake aitwae Vanila aliyepotea hivi karibuni.
Beautiful Onyinye, Wema Sepetu.
Akielezea ishu hiyo, Wema alisema mbwa huyo alikuwa na mwenzake
akiishi nao nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo
juzikati alikorofishana na mwenzake aitwae Thiona na kuamua kutokomea
kusikojulikana.
Mbwa wa Wema Sepetu aitwae Vanila.
Msanii huyo alisema anaomba yeyote atakayemuona Vanila wake
awasiliane naye au atoe taarifa kituo chochote cha polisi kilicho karibu
naye na atakabidhiwa pesa zake taslimu.


0 comments
Post a Comment